Uwekezaji katika sekta ya elimu Nchini kupitia mpango wa kuinua ubora wa
elimu (EQUIP-Tanzania) ambao umelenga kuboresha mchakato wa
kufundisha na matokeo ya kujifunza kwa watoto nchini umeweza kufanikiwa
kwa kiasi kikubwa Mkoani Simiyu.
Uwekezaji huo ambao unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia Wizara
ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) umeleta ufanisi wa elimu na
kufanya viwango cha ufaulu kuwa juu kutoka asilimia 36 mwaka 2013 mpaka
asilimia 68 2017.
Na katika kutimiza hayo Jumla ya kiasi cha shilingi Bil 1.7 kutoka DFID kupitia
mradi wa kuinua ubora wa Elimu Nchini (Equip) zimetolewa kwa Serikali ya
Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu
Mkoani humo .
Akizungumzia nia ya serikali ya Uingereza wakati wa mazungumzo na
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan , Mkuu wa DFID-Tanzania Elizabeth Arthy alisema wametoa
kiasi hicho cha fedha kwa serikali ya Mkoa wa Simiyu ili kuhakikisha
wanatatua changamoto ya miundombinu iliyopo.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Anthony Mtaka akimuelezea Makamu wa Raisi
utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi Elizabeth Arthy
akizungumza mbele ya makamu wa Rais juu ya mchango wa serikali ya Uingereza katika
kuboresha elimu.
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi Elizabeth Arthy
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shule ya msingi Gamondo A iliyoo wilayani Bariadi
mkoani Simiyu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...