Na Profesa Joseph Mbele
Ni furaha na faraja kwangu kama mwandishi kupata mrejesho kutoka kwa wasomaji. Leo asubuhi, nilipoamka, niliona ujumbe kutoka kwa mwalimu wa chuo cha St. Lawrence. Ameandika:

Mimi ni ndugu Kitito. Tulikuwa wageni wako katika kongamano la African network. Mimi na Robin tunashukuru mno kwa kitabu chako "Africans and Americans." Tunakitumia darasani mwetu. Wanafunzi wamefaidika mno...

Huyu mwalimu Robin anayetajwa nilishaandika habari zake katika blogu hii. Baada ya mimi kusoma ujumbe wake, mwalimu Kitito amenipigia simu, akanielezea zaidi kuhusu kitabu kinavyotumiwa. Nami nilimwelezea nilivyokiandika, baada ya miaka mingi ya kukabiliana na maisha ya Marekani. Nilimweleza kwa nini nilitumia mtindo ambao si kawaida kwa wanataaluma.

Nimefarijika kupata mrejesho kutoka kwa waalimu hao ambao wanatumia kitabu changu, nami nimeona niweke kumbukumbu hii hapa, kama ilivyo kawaida yangu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...