Na Emanuel Madafa-Mbeya
HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, imetoa siku saba kwa mkandarasi anayejenga nyumba ya serikali iliyoamuliwa na mahakama kuu kujengwa, kuibomoa baada ya kubainika kujengwa chini ya kiwango.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , Afisa habari wa halmashauri hiyo, John Kilua, amesema ofisi kupitia idara ya majengo ilitembelea eneo la nyumba hiyo inayojengwa kwa amri ya mahakama kuu na kubaini changamoto mbalimbali za ujenzi.
Amesema, kutokana na changamoto hizo wahusika wanaojenga nyumba hiyo wametakiwa kuibomoa na kuanza upya kwa kufuata kanuni za ujenzi na kwamba zoezi la kubomolewa kwa jengo hilo la nyumba linatakiwa kufanyika ndani ya siku saba.Nyumba hiyo yenye namba 1103/5 ambayo ipo katika eneo la Mafiat Jijini hapa, ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007 katika mahakama
Muonekano wa Nyumba yenye namba 1103/5 ambayo ipo katika eneo la Mafiat Jijini Mbeya , ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007 katika mahakama ya Wilaya Mbeya. 




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...