Na Saleh Jabir, UK

Nikiwa mwanafunzi ninayesomea sayansi ya kijamii, naandika makala hii kwa msukumo wa hisia ya uzalendo kwa nchi yangu na kwa kutumia maono yangu na akademia ya kisayansi kuhusu mambo ya kijamii yanayohusu jamii yetu kwa faida ya Watanzania wote. 

Uchambuzi wa moja kwa moja unaohusu jamii katika dunia hii ya leo ya utandawazi, utakuwa ni wa makosa iwapo hatujachambua siasa na uchumi kwa ujumla wake. Na uchambuzi wa moja kwa moja unaohusu siasa katika dunia hii ya leo ya utandawazi, utakuwa ni wa makossa iwapo hatujachambua uchumi na jamii kwa ujumla wake, na hali kadhalika. 
Kisayansi, utafiti na uchambuzi wa pamoja wa mambo yanayohusu jamii, siasa na uchumi ndiyo suluhisho la manufaa ya jamii ya karne ya 21 (21st century) na si vinginevyo.

Malengo ya makala hii ni kuangaza nchini kwetu Tanzania na kutolea mifano baadhi ya mataifa mengine ya jirani na ya mbali ambayo ni rafiki na Tanzania. Siyo kwasababu nyingine yoyote, ila ni kwasababu ya kuimarisha urafiki wa kweli na iwe ndiyo chachu ya maendeleo kwetu sisi kama Watanzania, kwa Afrika, na hata dunia nzima.
Tupo karne ya 21, na miaka 56 tangu tupate uhuru kutoka kwa mkoloni. Nchi yetu Tanzania inaelekea kubugikwa na utandawazi. Kipato cha mtu wa hali ya chini kimezidi kudidimia na kipato cha mtu wa hali ya juu kimezidi kuongezeka. Maadili kwa ujumla wake katika jamii yamezidi kuporomoka, na maadili katika utumishi wa umma kiasi fulani yameshuka. Tumeona baadhi ya wanasiasa, wanaharakati, na baadhi ya taasisi za kijamii zinatetea uovu na zinakemea yanayoonekana ni mema kwa faida ya jamii. Migongano ya kijamii yanayohusu ndoa za utotoni, ukeketaji na jinsia. Pia nitaelezea tofauti kati ya siasa na dini kisayansi. Yote haya ni changamoto za karne ya 21.
Makala hii ni yenye kuangalia athari ya utandawazi na siasa ya nchini kwetu Tanzania ili iwe ni kioo cha kuangalia wapi tunatoka, na iwe ni mizani ya kuangalia wapi tulipo, ili kwa umoja wetu, makala hii iwe ni moja ya mishale ya mwanga itakayoangaza mustakbali wa taifa letu na tunapoelekea. Ushauri wangu, mbali na kuisoma makala hii mpaka mwisho wake, makala hii iwe ni makala yenye kutusaidia kufikiri na kuzingatia yaliyomo ndani yake, kwasababu bila ya kujua wapi tunatoka, tutakuwa hatujui wapi tunaenda. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...