Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo amezitaka Halmashauri kuanzisha maduka ya
dawa katika wilaya zao ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa dawa kwenye
maeneo hayo.
Waziri Jafo ameitoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua duka la
dawa la kisasa lililofunguliwa katika Hospitali ya wilaya ya Kisarawe ambapo
duka linatarajiwa kuondoa tatizo la ukosefu wa dawa katika hospitali ya wilaya,
vituo vya afya, na zahanati wilayani Kisarawe.
Akifungua duka hilo, Jafo amesema endapo dawa zitakosekana
katika duka la hospitali au katika vituo vingine vya kutolea huduma ya afya
wilayani basi watanunua dawa katika duka hilo.
Aidha amezitaka Halmashauri zingine kuiga mfano wa Halmashauri
za Kisarawe, Muheza, Jiji la Tanga na zingine ambazo tayari zimejipanga vyema
kuwahudumia vyema wananchi wao katika suala la Afya.
Waziri Jafo ameipongeza Bohari ya Dawa(MSD) kwa msaada mkubwa
wanaoutoa katika kufanikisha uanzishaji wa maduka hayo ya dawa.
Duka hilo limeanzishwa kwa gharama ya sh. milioni 89 ambapo kiasi
cha Sh.Milioni 10 alizitoa Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe na Sh.Milioni
79 zilitolewa na Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa duka maalum la dawa Kisarawe.
Mganga Mkuu wa wilaya ya Kisarawe akitoa maelezo kuhusu uanzishaji wa duka la dawa wilayani humo.
1. Wananchi wa Kisarawe wakiwa katika ufunguzi wa duka la dawa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akikagua madawa yaliyohifadhiwa katika stoo ya duka la kisasa la dawa.
Stoo kubwa ya duka la dawa Kisarawe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...