Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango akiwa katika Picha ya Pamoja Ofisini kwake baada ya kutembelewa na Naibu Kamishina wa Polisi DCP Ahmada.A. Khamis Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii, Mkuu wa Kituo cha Polisi Nachingwea, SP Kasigwa, na Meneja Mwandamizi wa huduma za Uwakala Benki ya CRDB Bwa.Donath Mushi, Wengine ni Abel Laswai meneja mauzo wa wateja wadogo (wa kwanza kushoto) na Inspekta Issa Asali kutoka kitengo cha Polisi Jamii (wa mwisho kulia). Jeshi la Polisi pamoja na maafisa wa Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam wapo Mkoani Lindi kwa ajili kutoa elimu kwa umma juu Matumizi salama ya huduma za ki benk pamoja na elimu juu ya wizi wa fedha kwa njia ya mtandao.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango akimkabidhi zawadi ya Korosho kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo Naibu Kamishina wa Polisi DCP Ahmada.A.Khamis. Zawadi hiyo ilitolewa kama shukrani na wananchi wa wilaya hiyo kutokana na elimu waliyopewa.
Meneja Mwandamizi wa huduma za uwakala kwa Benki ya CRDB Donath Mushi akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Naipingu iliyopo wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, Jana juu ya matumizi salama ya Huduma za bank ma uhifadhi salama wa fedha katika benki hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...