Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini.
Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC, Tsvangirai mwenye umri wa 65 ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.
Taarifa ya kifo chame imethibitishwa na Makamu Rais wa chama chama cha MDC, Elias Mudzuri kupitia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kwamba marehemu alifariki jana jioni ya Februar 14.
Morgan Tsvangirai aliyekuwa ni mpinzani mkubwa wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe, alianzisha chama cha Movement for Democratic Change -MDC- mwaka 2000, na kuanza kutoa changamoto kwa Rais Mugabe aliyekaa madarakani muda mrefu.
Kufuatia kifo hicho cha Tsvangirai, chama cha MDC kinaweza kugawanyika juu ya nani atakayeongoza uchaguzi hapo baadaye mwaka huu dhini ya chama tawala cha Zanu PF, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Emmerson Mnangagwa.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...