KATIBU MKUU WA TLP, Mhe Nancy Mrikaria,anapenda kuwataarifu akina mama na akina baba kuwa Mhe.Augustino Lyatonga Mrema Mwenyekiti Wa Taifa wa bodi ya Parole na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa TLP atafanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika leo tarehe 01/02/2018 muda saa nane kamili mchana (8:00) katika viwanja vya stendi ya zamani ya mwenge.
Mhe Mrema,atamwaga sera na kumnadi mgombea Ubunge wa chama cha Tanzania Labour paty(TLP) Dr. Godfrey Malisa, watasikiliza shida ,KERO na changamoto za wananchi na kutoa suluhisho la matatizo ya wananchi wa jimbo la kinondoni,anawaomba wanakinondoni bila kujali chama kufika kwa wingi tusikilize sera za mgombea wao ,amekumbusha kuwa hii ni fursa ya wanakinondoni kusikiliza na kupima uwezo na sera bora ili kupata muelekeo wa kujua nani anastahili kuchaguliwa na nani anaweza kuwa mwakilishi wao makini na anayeweza kumaliza shida ZAO.
ikumbukwe kuwa UCHAGUZI NI tendo na utashi na itakuwa makosa IKIWA mwananchi atabaki nyumbani akiamini ATAKAYECHUGULIWA NI CHAGUO LA WOTE BILA YEYE BINAFSI KUPIMA NA KUJIRIDHISHA ATAKUWA ANAJINYIMA HAKI YAKE YA MSINGI.
KARIBUNI.
Imetolewa na ofisi ya Katibu MKUU,
chama cha TLP
MAKAO MAKUU - MAGOMENI
DAR ES SALAAM



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...