Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele amefunga mafunzo ya siku tano kuhusu msaada na huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii wanaosaidia kazi katika vituo vya huduma na tiba kwa watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) vilivyopo katika halmashauri 7 za wilaya mkoa wa Mwanza. 

Mafunzo hayo yalikuwa yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Midland Hotel jijini Mwanza kuanzia Jumatatu Februari 12,2018 hadi Ijumaa 16 Februari ,2018 yakiendeshwa na Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC). 

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Dk. Masele aliwataka wahudumu hao wa jamii kutumia vyema ujuzi na elimu waliyopewa ili wakaboreshe huduma za afya kwenye vituo vyao. "Nawashukuru AGPAHI kwa kutoa mafunzo haya,naamini mafunzo mliyopata yawatasaidia pia katika kuwaelimisha na kuwafuatilia wateja waliopotea katika huduma",aliongeza Dk. Masele. 

Nao washiriki wa mafunzo hayo, Hawa Radhamani kutoka hospitali ya wilaya ya Misungwi Kija Robert kutoka kituo cha afya Nyamilama halmashauri ya wilaya ya Kwimba walisema wamepata uelewa mkubwa kuhusu masuala ya VVU na Ukimwi yatawasaidia kuboresha zaidi huduma za afya kwenye vituo vyao na jamii kwa ujumla. 
Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele akifunga mafunzo ya siku tano kuhusu msaada na huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii kutoka halmashauri za wilaya mkoa wa Mwanza.
Dk. Masele akikabidhi cheti cha ushiriki kwa Sospeter Lameck kutoka halmashauri ya wilaya ya Buchosa.Wa kwanza kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona. Wengine wawezeshaji wakati wa mafunzo hayo Dk. Joseph Musagasa (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Gaston Kakungu ambaye ni Afisa Muuguzi Mstaafu.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akifundisha namna ya kujaza taarifa katika daftari la mtoa huduma za VVU na Ukimwi katika jamii. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakijaza fomu ya namna ya kufuatilia wateja waliopotea katika huduma. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...