Mwakilishi wa TatuMzuka,Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi Bi Neema Mtewele (38),ambaye ni mfanyabiashara wa nguo za akina mama Kariakoo jijini Dar Es Salaam,aliyeibuka na kitita cha shilingi milioni 60 za TatuMzuka mwishoni mwa wiki.
Neema Mtewele (38),ambaye ni mfanyabiashara wa nguo za akina mama Kariakoo jijini Dar Es Salaam,akifafanua mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyofanikiwa kushinda mamilioni hayo ya Mchezo wa kubahatisha wa Tatumzuka.Neema alisema kuwa amekuwa akiucheza muda mrefu mchezo huo bila mafanikio,lakini hakukata tamaa,alindelea kucheza na hatimae akabahatika kuibuka mshindi wa milioni 60.
"Hizi fedha kwakweli matumizi yake makubwa yatakuwa ni kuendeleza na kuunyanyua zaidi mtaji wangu niliokuwa nao kwenye biashara yangu,bado nahitaji kuikuza zaidi biashara yangu",alisema Neema huku akionesha furaha ya wazi kwa kushinda kitita hicho cha milioni 60.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...