Na Genofeva Matemu –
WHUSM
Msanii wa filamu
nchini Bibi. Wastara Issa ameendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha moyo wa kuguswa na tatizo
linalomsumbua na kuweza kumpatia kiwango cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya
matibabu ya mguu pamoja na mgongo.
Bibi. Wastara ametoa
shukrani hizo leo Jijini Dar es Salaam alipokua akizungumza na waandishi wa
habari na kusema kuwa awali ilikua aondoke nchini tarehe 28 mwezi januari mwaka
huu kwenda mjini Mumbai kwa ajili ya matibabu lakini kutokana na baadhi ya
mipango kutokaa vizuri safari hiyo ilisogezwa hadi jumapili tarehe 4 Februari
2018 ambapo anatarajia kuondoka mida ya jioni na kufika Mumbai mapema alfajiri siku
ya jumatatu ambapo ataanza matibabu siku hiyo hiyo.
Bibi. Wastara amesema
kuwa katika safari hiyo ataongozana na nesi mmoja kutoka hospitali ya TMJ
pamoja na mtu mmoja kutoka katika familia yake ambapo matibabu yake yatafanyika
katika hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai na kutarajia matibabu hayo kuchukua
takribani wiki tatu na zaidi.
Aidha msanii Wastara
Issa ameishukuru wizara inayosimamia tansia ya filamu kwa kumfariji katika
kipindi hiki kigumu anachopitia huku akimshukuru Waziri mwenye dhamana na
tasnia ya filamu nchini, Bodi ya Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa la Taifa pamoja
na watanzania wote kwa kuonyesha upendo wa dhati kwake.
“Asanteni sana
watanzania mmeonyesha moyo wa dhati kwangu kwa muda mrefu sasa, mmekua pamoja
nami tangu kipindi cha matibabu ya Saduki hadi sasa, uzito wa neno asante
kutoka kwangu leo hauwezi kulipa fadhila kwa dua na michango yenu kwangu,
mwenyezi mungu aendelee kuifanya nchi yetu kuwa na amani na upendo” amesema
msanii Wastara Issa
Naye Katibu Mtendaji
Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa serikali kupitia bodi ya filamu inashukuru
kwa kupata taarifa kamili ya safari ya msanii Wastara Issa ilipofikia kwani
bodi ya filamu inapenda kumuona Wastara akiwa katika afya nzuri na kurudi katika
hali yake ili aweze kuungana na wanatasnia wenzake kuendeleza tasnia ya filamu
nchini.
Bibi. Fissoo amesema
kuwa Watanzania wengi wamekua wakiwasiliana na Wastara kwa njia mbalimbali,
kumchangia na hata kufika kumuona, hivyo serikali inatambua kuwa msanii Wastara
Issa yupo katika maandalizi ya safari ambapo awali alikua asafiri tarehe 28 mwezi januari mwaka 2018 lakini
kutokana na taratibu za safari kutokukamili kumepelekea safari hiyo kusogezwa
hadi tarehe 4 februari mwaka huu.
Msanii wa Filamu
nchini Bibi. Wastara Issa (wapili kulia waliokaa chini) akizungumza na
waandishi wa habari nyumbani kwake kuhusu maandalizi ya safari
yake ya matibabu kuelekea Mjini Mumbai walipofanya naye mazungumza leo Jijini
Dar es Salaam. Watatu kulia waliokaa ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi.
Joyce Fissoo



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...