Na Yusuph Mussa, Korogwe
Mzee Stephen Hizza (pichani), mtunzi na muimbaji wa wimbo "TANZANIA YETU NI NCHI YA KUPENDEZA", ambao aliutunga na kuimba mwaka 1966 akiwa na bendi ya Atomic Jazz ya mkoani Tanga, wakati Taifa letu linafikisha miaka tano tangu tupate Uhuru mwaka 1961, amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wodi ya Kibasila namba 14 akiwa anaumwa Tezi Dume.
Nilihojiana nae mwaka 2011 kwa kumfuata Jiji la Tanga wakati Taifa letu linatimiza miaka 50 tangu kupata Uhuru.
Hakika mzee huyu ni moja ya HAZINA yetu kutokana na utunzi wa wimbo huo ambao unahamasisha uzalendo na kuipenda nchi yetu.
Ombi kwa Watanzania, mwenye chochote ambacho anadhani kitamsaidia kupata afueni, basi amsaidie kwa kutumia namba hii 0657-513067.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...