Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akijadiliana jambo na Majaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika ya Mashariki (EACJ) wakati alipoitembelea mahakama jijini Arusha Ijumaa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dk, Adelardus Kilangi akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ( EACJ), Mhe Jaji Dk. Emmanuel Ugirashebuja na katika mazungumzo yao Rais wa EACJ alimweleza Mwanasheria Mkuu kwamba mahakama hiyo imekuwa ikizitegemea Ofisi za Wanasheria Wakuu ikiwamo ya Tanzania katika utekelezaji wa Majukumu yake.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dk. Adelardus Kilangi akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Watu na Binadamu (AfCHPR) Jaji Sylvain Ore walipokuta Jijini Arusha. Katika mazungumzo yao, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliahidi kushirikiana wa Mahakama hiyo ambapo kwa upande wake Rais wa AfCHPR alisema mahakama hiyo imekuwa ikipata ushirikiano mzuri kutoka kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia kwa Mawakili wa Serikali ambao wamekuwa wakiiwakilisha serikali katika mashauri mbalimbali.. Mwingine katika picha ni Katibu wa Mwanasheria Mkuu, Wakili wa Serikalil Mkuu Ephery Sedekea.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiangalia namna mfumo wa habari na mawasiliano wa mahakama hiyo unavyofanya kazi wakati alipoitembelea Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki leo Arusha
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...