Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kujitangaza umuhimu wake katika nyanja ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi na taifa kwa ujumla. 

Mhandisi Nditiye ameyasema hayo alipotembelea makao makuu ya TMA na kuzungumza na bodi ya Mamlaka hiyo, menejimenti na wafanyakazi kwa lengo la kutambua majukumu yao na kufuatilia utekelezaji wake ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwatumikia wananchi.

Akizungumza na Bodi, menejimenti na wafanyakazi, Mhandisi Nditiye amewaeleza kuwa TMA ni chombo muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya taifa letu na wananchi kwa ujumla kwa kuwa sekta ya usafiri wa anga, majini, ujenzi wa majengo mbalimbali, miundombinu ya barabara na reli, afya, kilimo na mazingira vyote vinategemea taarifa za hali ya hewa kutoka kwenye Mamlaka hii. 

“Mtambue kuwa hakuna ndege inayoweza kutua wala kuruka bila kupata taarifa kutoka kwenu, vile vile mkandarasi anayejenga reli ya kisasa ya SGR nae anategemea taarifa zenu kwa kiasi kikubwa, hivyo mtambue ninyi ni muhimu na mjitangaze,” amesema Mhandisi Nditiye.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akizungumza na Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati alipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dkt. Hamza Kabelwa
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiy (hayupo pichani) akiangalia picha za usafiri wa anga na majini ambazo usafiri wake unategemea utabiri wa hali ya hewa wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akipatiwa taarifa ya hali ya hewa kwa usafiri wa anga na Meneja wa Utabiri wa Hali ya Hewa Bwana Samwel Mbuya wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati alipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...