Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma jana jioni aliamua kujiuzulu wadhifa wake huo kufuatia kuongezeka kwa shinikizo la kumtaka afanye hivyo kutoka kwa chama chake cha ANC (African National Congress) , kinachotawala nchini humo kufuatia miaka 9 ya kukabiliwa na kashfa za rushwa, kuporomoka kwa uchumi na kushuka kwa umaarufu.

Awali kabla ya kuamua kug'atuka kwake kwenye wadhifa huo wa juu kabisa nchini humo, Rais Zuma alikilalamikia chama chake cha ANC kwa kumtaka aondoke madarakani, ikiwa ni pamoja na kumtishia kumuondoa kupitia kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye, iliyopangwa kupigwa hii leo, Alhamisi.

Rais Zuma amesema anaheshimu maagizo ya chama chake cha ANC kwa kumtaka kujiuzulu wadhifa wake, baada ya wiki kadhaa za uvumi kuhusu mustakabali wake. Alinukuliwa akisema “nimeamua kujiuzulu kutokana na kura ya kutokuwa na Imani iliyokuwa imepangwa kupigwa siku ya Alhamisi".

Katika hotuba ya kitaifa aliyoitoa kwa dakika 30 kupitia tekevisheni mbalimbali nchini humo, Zuma alisema, hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja. 

Zuma amekuwa katika mvutano wa kimadaraka na mfanyabiashara bilionea wa zamani na makamu wa rais, Cyril Ramaphosa ambaye sasa anakuwa rais wa mpito. Ramaphosa aliyeshinda nafasi ya kukiongoza chama cha ANC, baada ya kuchaguliwa mwezi Disemba, atapigiwa kura na wabunge nchini humo kuwa rais mpya wa mpito kati ya leo au kesho Ijumaa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...