Na Agness Francis, Globu ya jamii
MBUNIFU wa mavazi nchini Ally Rehmtulah ameweka wazi mafanikio na changamoto alizopitia ndani ya miaka 10 katika kuendeleza sanaa ya ubunifu hapa nchini..
Akizungumza nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Rehmtulah amesema Mama wa mitindo nchini Asia Idarous ndiye aliyeng'arisha nyota yake kwa kumshika mkono kwa kumpa fursa ya kwanza kuonesha shoo ya mavazi yake kwa watanzani katika tamasha la Lady in read.
"Baada ya hapo watanzania walianza kunikubali ndio nikaanza kufanya shoo zangu sehemu mbalimbali ikiwepo kusafiri nje ya nchi nilihangaika sana kuanza kushona nguo.
"Naenda Kariakoo kutafuta vitambaa na mafundi popote pale wa kushona nguo, vile vile pia nilifanikiwa kufanya kazi Landani fashion week,Rwanda, Uganda na Kenya.Hiyo yote ni kuhangaika tu kutafuta soko sehemu tofauti tofauti,"amesema Rehmtulah.
Aidha amesema tokana na changamoto hizo imemfanya kufungua kampuni yake ya kiwanda cha utengenezaji wa nguo kwa kuona anapata oda nyingi kutoka nje ambapo haikuwa na uwezo wa kuweza kukamilisha oda hizo kutokana na ukosefu wa viwanda hapa nchini.
"Nimeamua kuanzisha kiwanda kidogo ilikuweza kukamilisha ubora wa oda nazopata kutoka soko la nje.
"Na hadi mpaka sasa naimeajiri watu 11 unafanyanao kazi nawalipa kwa wakati nalipa kodi na hata NSSF kwa kila mfanya kazi wangu,"amesema Rehmtulah.
Mwanamitindo Ally Rehmtulah akizungumzia mafanikio na changamoto aliyoyapitia ndani ya mika 10 ya tasnia ya ubuni wa mavazi leo Nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam..



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...