Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WIZARA ya Madini imetangaza kuanzia sasa mnada wa madini yote utafanyika hapa nchini badala ya nje ya nchi kama ulivyokuwa unafanyika awali.

Lengo ni kuizesha Serikali kupata mirabaha yake pamoja na wachimbaji kuwa na uhakika wa soko la madini.

Uamuzi huo umetokana na mnada wa madini uliofanyika nchini Ubelgiji ambapo jumla ya karati 54,094.47 ziliziuzwa kwa dola za Kimarekani 13,607,858.72 sawa na Sh.bilioni 30.6.Mnada huo ni watatu wa madini ya Almasi ya mgodi wa Mwadui mkoani Shinyanga .

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Naibu  Waziri wa Madini,  Dotto Biteko amesema mnada huo kufanyika hapa nchini utailetea nchi faida katika mapato yatokanayo na madini .

Amezitaja faida ni kuongezea nchi mapato yatakayotakana na wageni kuja kwenye mnada huo wa madini pamoja na kuikuza nchi kwenye sekta ya madini.

Amesema hapo awali mnada ulipokuwa unafanyika nchini Ubeligiji, Taifa lilikuwa linapoteza fedha nyingi kutokana na makampuni mengi ya madini kufanya udanganyifu kwenye uuzaji wa madini.

Biteko amesema amesema ujenzi wa ukuta kwenye mgodi wa Mererani mwenye urefu wa kilomita 24.5 ambao upo hatua za mwisho kukamilika.

Pia, Serikali imesema Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kushirikiana wataalam wa Wizara ya Madini wataanza kutoa vitambulisho vya uraia kwa wananchi wa eneo la Mererani ambao ni wachimbaji wadogowadogo wa madini ili waweze kufanya uchimbaji kama sheria inavyotaka.
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mnada wa madini uliofanyika nchini Ubelgiji na serikali kuweza kupata mauzo mazuri leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...