Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
RADIO Uhuru imeandaa show MIC TATA itakayowashirikisha wasanii mbalimbali nchini itakayofanyika Februari 24 katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa Uhusiano , Sheila Simba amesema kuwa show siyo ya kukosa kutokana na wasanii walivyojipanga katika kukutanisha wasanii mbalimbali .
Sheila amesema kuwa radio uhuru kufanya show hiyo ni mwendelezo wa show zingine ikiwa ni kukutanisha wasanii mbalimbali kutoa burdani kwa mashabiki wao.Wasanii watakaotumbiza katika Mic Tata ni Joe Makini , Inspekta Haruni , Manifongo , Dulla Makabila na Amigo wa Tarabu huku kiingilio ikiwa ni sh. 5000


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...