TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevikumbusha vyama
vya siasa ambavyo vimesimamisha wagombea ubunge na udiwani katika majimbo
mawili na kata tisa kuwa kesho (Februari 10) ndio siku ya mwisho ya kuwasilisha
orodha ya mawakala wao kwa wasimamizi wa uchaguzi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Bw. Ramadhan Kailima
amesema hatua hiyo ni kwa mujibu wa kifungu namba 57 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi
(Sura ya 343) na kifungu namba 58 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa
(Sura ya 292) ambazo zinabainisha kuwa majina ya mawakala wa vyama vya siasa yanatakiwa kuwasilishwa
kwa msimamizi wa uchaguzi siku saba kabla ya uchaguzi.
“Uchaguzi utafanyika tarehe 17 Februari 2018, hivyo
siku saba kabla ya uchaguzi ni kesho (tarehe 10 Februari), hivyo nivisihi vyama
vyote vya siasa vilivyosimamisha wagombea, kama vikitaka kuweka mawakala kwenye uchaguzi huo, vipeleke orodha yao yaani
utambulisho wa barua na kesho Jumamosi ndio siku ya mwisho.
“Ikifika tarehe 11 yaani Jumapili wasimamizi wa uchaguzi
hawataruhusiwa kupokea orodha ya mawakala wa vyama vya siasa,” amesisitiza
Kailima na kuongeza kuwa orodha hiyo ya mawakala kwa mujibu wa sheria iwe
inaonesha jina la wakala, anuani yake na kituo ambacho chama kimependekeza wakala
aende kusimamia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...