Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa msaada wa Komputa aina ya Laptop 200 kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo.

Laptop hizo zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 400 zimetolewa ikiwa ni mwendelezo wa UNICEF kuiunga mkono Serikali katika kuimarisha huduma za matibabu hasa ya akinamama na watoto.Akikabidhi Msaada huo katika Ukumbi wa Wizara hiyo Mnazi mmoja Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Francesca Morandin amesema upatikanaji wa taarifa sahihi ni jambo muhimu linalofaa kupewa kipaumbele.

Amesema uwepo wa taarifa sahihi za Wajawazito na watoto huisaidia Serikali kujua idadi ya ongezeko la watu wake hali inayopelekea kupanga mipango vyema ya matibabu kulingana na idadi ya watu husika.Amewataka Watendaji kwa ujumla kuunga mkono juhudi zinazotolewa na UNECO ili kuhakikisha afya za Watoto na Wajawazito zinaimarika.

Francesca ameongeza kuwa Shirika hilo la UNICEF litaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika juhudi zake za kimatibu na kuipongeza Srikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kutoa matibabu bure kwa wananchi wake.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo kushoto na akikabidhiwa Msaada wa Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kutoka kwa Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Francesca Morandin ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Francesca Morandin akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Msaada wa Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kwa Wizara ya Afya Zanzibar ili zisaidie kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...