Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha kiasi cha Dola za Marekani 150,000 inayomkabili Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania Maputo nchini  Msumbiji, Joyce Moshi (56) bado haujakamilika.

Mshtakiwa Moshi anayeishi Temeke anakabiliwa na mashtaka tisa yakiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, wizi akiwa mtumishi wa umma na utakatishaji wa fedha.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa kwani upelelezi bado haujakamilika na wanasubiri nyaraka kutoka  Msumbiji ili kukamilisha upelelezi. Hakimu Shaidi ameutaka upande wa mashtaka kuendelea kufuatilia hizo nyaraka ili upelelezi ukamilike na kesi imeahirishwa hadi Machi 13, mwaka 2018.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa  Oktoba 25, mwaka 2016 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Maputo nchini Msumbiji alighushi barua ya Oktoba 25, mwaka 2016.

Akijaribu  kuonesha kuwa ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji imeilekeza Benki ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha  dola za Marekani 10,000 kutoka kwenye akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Mushi na akaunti hizo zote  zipo kwenye benki hiyo iliyopo katika tawi la Julius Nyerere Maputo, wakati akijua si kweli.

Anadaiwa kuwa Februari 10, mwaka 2017 katika ofisi za Ubalozi Maputo Msumbiji, alighushi barua akionyesha  kuwa ubalozi huo umeielekeza Benki ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha dola za Marekani 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Moshi.

 Aprili 12, mwaka 2017 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania  Maputo nchini Msumbiji, mshtakiwa huyo anadaiwa alighushi barua ya Aprili 12, mwaka 2017 akijaribu kuonesha kuwa ubalozi huo umeielekeza Benki  ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha dola za Marekani 40,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177.

 Oktoba 25, mwaka 2016 katika Benki ya Millennium BIM iliyopo tawi la Julius Nyerere Maputo nchini Msumbiji, aliwasilisha kwenye benki hiyo nyaraka za kughushi ambayo ni barua ya Oktoba 25, 2016 akionesha kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji umeelekeza benki hiyo kuhamisha dola za Marekani 10,000 kutoka kwenye akaunti ya benki hiyo kwenda kwenye akaunti inayomilikiwa na mshitakiwa huyo.

Iliendelea kudai kuwa Februari 10, 2017 katika benki hiyo, Moshi alitoa nyaraka za uongo kuonesha kwamba Ubalozi umeelekeza kuhamisha dola za Marekani 10,000 kwenda kwenye akaunti ya Moshi.

 Aprili 12, 2017 katika maeneo ya benki hiyo mshtakiwa huyo aliwasilisha barua ya Aprili 12, 2017 kuonesha kuwa ubalozi umeelekeza kuamisha dola za Marekani 40,000 kwenda kwenye akaunti ya Moshi.

Katika tarehe tofauti kati ya Oktoba 25,mwaka 2016 na Aprili 12, mwaka 2017  akiwa mtumishi  wa umma kama Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, aliiba dola za Marekani 150,000 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inadaiwa kati ya Oktoba 25, 2016 na Aprili 12, 2017 katika ofisi za ubalozi huo, Moshi alijipatia dola za Marekani 150,000.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa,  kati ya Oktoba 25, 2016 na Aprili 12, 2017 katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania uliopo Maputo nchini Msumbiji na Benki ya Millenium BIM tawi la Julius Nyerere Maputo, alijipatia dola za Marekani 150,000 wakati akijua fedha hizo ni zao la  kughushi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...