Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, upelelezi wa kesi ya mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, Wayne Lotter (52) inayomkabikabili Meneja wa benki Khalid Mwinyi (33) bado haujakamikika.

Wakili wa Serikali, Adolf Mkini ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Wakili Mkini alidai kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ili kuona kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Kabla ya Wakili huyo kueleza hayo, mshtakiwa Rahma Almas aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa Mohammed Maganga anaumwa na yupo gerezani.

Washtakiwa wengine  katika kesi hiyo ni Rahma Almas maarufu kama Baby (37)  Mfanyabiashara na Mohammed Maganga mwenye (61) ambaye ni mchimba makaburi.

Kesi imeahirishwa hadi Machi 6,mwaka 2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la mauaji ambapo wanadaiwa, Agosti 16,mwaka 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie Kinondoni Dar es Salaam, ambapo walimuua Lotter.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...