Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kampuni ya King Lion imetoa msaada wa waendesha bodaboda  waliopata ajali na wamelazwa katika Hospitali Taifa ya Muhimbili

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukakabidhi  msaada huo Afisa Uhusiano na Masoko, Erasto Baragamba amesema kuwa kama kampuni inatambua umuhimu wa waendesha bodaboda  hivyo wanatoa mchango ambao utasaidia kujisitili.

Msemaji wa waendesha bodaboda Wilaya ya Ilala, Abdallah Bakari amesema wanashukuru kinglion kwa msaada walioutoa.

Amesema waendesha bodaboda wazingatie sheria za usalama barabarani ili kuweza  kuepukana na ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu.
 Msemaji wa waendesha bodaboda wa Manispaa ya Ilala, Abdallah Bakari akizungumuza  na waandishi  habari kuhusiana msaada kwa waendesha bodaboda waliopata ajali na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Msemaji wa waendesha bodaboda wa Manispaa ya Ilala, Abdallah Bakari  akikabidhiwa msaada kutoka kwa Afisa Uhusiano na Masoko, Erasto Baramamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...