ASASI ya kiraia ya Financial Education for Development and human Achievement (FEDHA) Machi 28 mwaka huu kuzindua mradi wake juu ya kuelimisha vijana kuhusu udhibiti sahihi wa pesa binafsi katika nyanja za utafutaji na utumiaji pesa, uwekaji akiba, uandaaji wa bajeti na uwekezaji wa pesa ili kuwawezesha kukuza ustawi wao wa kipesa na kufikia uhuru wa kifedha.
Hayo ameyasema Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa
Akizungumza kuhusu asasi ya FEDHA, Bw. Jafari Selemani – Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo amesema “Asasi ya kiraia ya FEDHA ni asasi pekee ambayo imejikita katika utoaji wa elimu ya udhibiti pesa binafsi ili
kukuza uelewa wa masuala ya kifedha kwa umma wa watanzania kuanzia ngazi ya chini yaani wakiwemo watoto, vijana hadi watu wazima, dhima yetu ni kuwafanya watanzania wapate ujuzi,weledi na taarifa sahihi
juu ya masuala ya kifedha ambapo itawasaidi kufanya maamuzi ya kujiamini yenye manuufaa kwao binafsi na kwa nchi katika kuhakikisha tunapata sekta ya fedha na uchumi imara na endelevu”
“Malengo ya FEDHA ni, kukuza ustawi wa
kipesa kwa kutoa elimu; kuwezesha watanzania kutambua wajibu na haki zao kama watumia wa bidhaa na huduma za kifedha; kushiriki kuleta ujumuishi wa uchumi na kifedha Tanzania; na Kushirikiana na wadau
mbalimbali katika kupambana na Umasikini pamoja na udhibiti finyu wa rasilimali fedha.” amesema Selemani.
Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo pamoja na kutambulisha mradi wa "Viepe" kwa kutoa elimu kwa vijana wa sekondari kakika mkoa wa Dar es Salaam na baadae Tanzania kwa ujumla.
Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu wa FEDHA, Mohamed Mchoro na kushoto ni Afisa mradi wa FEDHA, Linus Amedei.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...