Na Benny Mwaipaja, Kondoa.
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma kutenga fedha kwenye bajeti ya Mwaka ujao wa Fedha 2018/2019 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Kondoa ili kukabiliana na changamoto za afya zinazowakabili wananchi.
Dkt. Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wakati akianza ziara yake ya siku mbili wilayani humo kukagua shughuli za maendeleo zinazotokana na fedha zilizotolewa na Serikali ikiwemo ujenzi wa vituo vipya vya afya pamoja na miundombinu ya elimu wilayani humo.
Alisisitiza kuwa atafuatilia na kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa ili kusogeza huduma ya afya karibu zaidi na wananchi hususan waishio vijijini ambao wanakosa huduma ya uhakika kutokana na kukosekana kwa hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Kondoa.
Aidha, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amewataka watendaji wa halmashauri hiyo ya Wilaya ya Kondoa kuhakikisha kuwa wanawatumikia wananchi kwa moyo, umoja na mshikamano ili malengo ya kitaifa ya kuwaletea maendeleo kupitia dhana ya Tanzania ya viwanda yaweze kufikiwa.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Kondoa Vijijini Dkt. Ashatu
Kijaji (kulia) akielezea maendeleo ya viwanda katika Halmashauri hiyo
kwa kusisitiza kujikita katika kilimo ili kupata malighafi wakati wa
Mkutano na viongozi wa Idara mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya
Kondoa.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Falesy Mohamed Kibassa (wa pili
kulia) akipongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango na Mbunge wa Kondoa Vijijini Dkt. Ashatu Kijaji (kulia)
katika kufanikisha maendeleo ya Wilaya hiyo wakati wa Mkutano kati yake
na viongozi wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Kondoa Vijijini Dkt. Ashatu
Kijaji (kushoto) akizungumza jambo na Afisa Elimu Sekondari wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bi. Hilda Saganda (kulia) baada ya
kumalizika kwa Mkutano kati ya Naibu Waziri huyo na viongozi wa idara
katika Halmashauri hiyo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...