Wananchi wanaozunguka mgodi wa madini ya chumvi ya Gendabi Wilayani Hanang' wanatarajia kunufaika na rasilimali hiyo, baada ya Serikali kupata mwekezaji atakayejenga kiwanda cha chumvi eneo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza jana kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano wilayani humo alisema atawachukulia hatua kali wanasiasa watakaokwamisha mradi huo. Mnyeti alisema wapo baadhi ya wanasiasa wanaotumia matatizo ya wananchi kuwa fursa hivyo hawezi kukubali wakwamishe mradi huo mkubwa wenye faida kwa jamii.

"Nimesikia hapa kuna baadhi ya wanasiasa wanatumia shida za watu kujinufaisha kisiasa, sasa nikimkuta anapinga hili nitamshughulikia bila kujali chama chake,," alisema Mnyeti. Alisema kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji hivyo wananchi wa eneo hilo wajiandae kunufaika kiuchumi kwa kuchimba chumvi kwa wingi na kuuza kiwandani hapo.

"Haya ndiyo maendeleo tunayosema siyo siasa za maji taka kwani chumvi itakuwa na thamani kubwa tofauti na hivi sasa kwani kiwanda kitawanufaisha," alisema Mnyeti. Aliwataka wananchi wa eneo hilo kujiweka tayari na uwekezaji huo ili kuhakikisha uzalishaji unafanyika wa kutosha kwani soko la uhakiki litakuwepo kwa kadiri watakavyofanya uzalishaji.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akiangalia kiatu kilichotengenezwa na kikundi cha Datoga cha Wilayani Hanang kinachotengenezwa vifaa vinavyotokana usindikaji wa ngozi.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akipokea heshima kutoka kwa skauti mara baada ya kuwasili Wilayani Hanang jana alipoanza ziara ya siku tano, ya kutembelea wilaya hiyo kwa kuzungumza na wananchi, kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero zao. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, (kushoto) akizungumza jana kwenye eneo la kuhifadhi dawa baada ya kukagua mazingira ya hospitali ya Wilaya ya Hanang kwenye ziara yake ya siku tano.  


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...