Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MBUNGE wa Ubungo Mhe. Saed Kubenea, amewasilisha bungeni hoja binafsi, kutaka kufanyika mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ili kuruhusu kuundwa kwa “Tume Huru ya Uchaguzi.
Kubenea ambaye leo amewaita Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kuwaeleza kwanini ameamua kupeleka muswada huo katika bunge hili linaloanza Aprili 1, 2018.
 Mhe. Kubenea amesema, uchaguzi huru na haki hauwezi kufanyika nchini bila kuwapo na chombo huru cha kusimamia na kuendesha chaguzi hizo.
“Hoja kwamba NEC siyo chombo huru, siyo maneno yangu pekee. Haya yameelezwa vizuri na wanazuoni mbalimbali, ikiwamo Tume ya Jaji Francis Nyalali ambayo iliundwa na Rais wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, mwaka 1991.tume hii ya Jaji Nyalali ndio iliyokuja kupendekeza kuwapo kwa mfumo wa vyama vingi nchini,’’Amesema Kubenea.
 Aliongeza kuwa mwaka 1999, Tume iliyoundwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuratibu maoni ya wananchi kuhusu Katiba ilipigilia msumali mwingine kuhusu muundo wa sasa wa NEC iliyoongozwa na Jaji Robert Kisanga.
Kwenye ripoti ya Jaji Kisanga alisema “hatua ya wajumbe wa Tume kuteuliwa na Rais ambaye pia aweza kuwa kiongozi wa chama cha siasa kinachotawala, katika utendaji wao wa kazi ama watakuwa na upendeleo kwa chama husika au watakuwa wanalipa fadhila 
 Mbunge wa Ubungo Mhe. Saeed Kubenea akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Hoja yake aliyowasilisha bungeni kutaka iundwe  tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
 Mbunge wa Bukoba Mjini  Mhe. Willfred Rwakatale, akichangia jambo wakati Kubenea alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kuwasilisha hoja ya kuwepo kwa tume huru ya Uchaguzi.
 Mbunge wa Moshi Vijini Mhe. Antony Komu  akichangia jambo baada ya Kubenea kuzungumza na Waandishi wa Habari juu kuwasilisha Hoja Binafsi.
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioudhuria Mkutano huo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...