Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MEYA wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Charles Kuyeko amewataka wenyeviti wa Serikali za mitaa wilayani humo kuacha kuwatoza fedha wananchi  wanaofika katika ofisi zao kupata huduma kwani kufanya hivyo tafsiri yake ni rushwa.

Meya Kuyeko amesema hayo leo asubuhi alipokuwa akifungua ofisi mpya ya Serikali ya mtaa wa Mtakuja iliyopo katika kata  Vingunguti Ilala jijini ambapo amesisitiza umuhimu wa viongozi wa ngazi mbalimbali kutoa huduma kwa wananchi bila kuomba fedha.

"Utekelezaji wa majukumu ya ofisini, ninaomba tusiombe rushwa wananchi wanaohitaji huduma.Viongozi endeleeni kushirikiana na wananchi ili kazi ziendelee.Nishauri wananchi msikae na vitu moyoni, mnapaswa kupaza sauti kwa jambo lolote ili lipatiwe ufumbuzi,"amesema Kuyeko.

Kwa upande wa Diwani  wa Kata ya Vingunguti na Naibu Meya wa Manispaa hiyo , Omary Kumbilamoto amemshukuru Meya kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo ambayo italeta tija kwa wananchi waishio maeneo hayo kwani kabla ya hapo walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma kwa Mwenyekiti.

Aidha amemshukuru  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo kwani kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini( TARURA) amekubali kuifanyia matengenezo barabara ya Vingunguti kwa Mnyamani.

Amefafanua barabara hiyo imechimbika na hivyo kuwa na mashimo mengi kiasi cha kuifanya kutopitika kwa urahisi na hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na msongamano mkubwa wa magari yanayosababishwa na ubovu wa barabara.

Pia amemuonya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtakuja asigeuze ofisi hiyo mpya ya Serikali ya mtaa kuwa mahabusu kwa kunyanyasa wananchi wasiokuwa na hatia,hivyo watu wote watakaokamatwa wapelekwe kwenye vyombo vya kisheria.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akifungua ofisi mpya ya Serikali ya Mtaa wa Mtakuja kata ya Vingunguti ambayo imejengwa kwa gharama za Halmashauri hili kuweza kuleta huduma jirani na Wananchi.kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Omary Kumbilamoto akishuhudia uzinduzi huo.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza na wakazi wa Vingunguti kuhusu umuhimu wa ofisi hiyo na kusisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutoa taarifa za rushwa wanazoombwa na Viongozi.
 Diwani wa Kata ya Vingunguti  na Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Omary Kumbilamoto akitoa nasaha zake kwa wakazi wa Vingunguti mara baada ya uzinduzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mtakuja.
 Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mtakuja inavyoonekana kwa nje, mara baada ya kujengwa  na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa gharama ya Shilingi Milioni 45 .
Sehemu ya Wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa ofisi ya Serikali  ya Mtaa wa Mtakuja ambayo imejengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...