Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii
MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameigizaa Bodi ya Barabara kuhakikisha fedha za  mkopo ambazo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara zinatumika ipasavyo

Amesema fedha hizo zinatakiwa kujenga barabara za kisasa na si  kutumika kwenye warsha, semina na safari za mafunzo nje ya nchi.

 Akizungumza leo, Makonda amesema Dar es salaam ina fedha za DMDP takribani Sh.bilioni 600 kwa ya kujenga barabara na mifereji lakini asilimia kubwa ya fedha hizo zimekuwa zikitumika kwenye semina na safari za nje ya nchi kujifunza namna ya usimamizi wa barabara.

"Jambo jambo linalosaabisha Serikali kulipa madeni kwa mirado ambavyo imekusudiwa," amesema Makonda.

 Pia Makonda  amegundua gharama ya kujenga barabara ya Kilometa moja kwa fedha ya DMDP ni sawa na gharama ya kujenga barabara ya TANROAD Kilometa 3, hivyo ameshauri kikao hicho kuangalia kwa umakini jambo hilo ili fedha hizo ziweze kuleta tija kwa wananchi kwa uwepo wa barabara zenye ubora.

Amesema kwa mwaka wa fedha wa 2018-2019 Mkoa wa Dar es salaam umetenga Sh.bilioni 289.3 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Wakala wa Barabara za Mijini na Vijini(TARURA),Tanroad na vyanzo  Wakala wa Barabara za Mjini na vya ndani vya halmashauri.

Ameongeza  hataki kuona w,ananchi wa Dar es Salaam wanateseka kutokana na ubovu wa barabara zenye mashimo na mahandaki.

Amesema hali hiyo husababisha hasara ya uharibifu wa vyombo vya usafiri na wakati mwingine ongezeko la msongamano wa magari.

"Nimeanza kuona nuru baada wakandarasi wa barabara za Dar es salaam kuanza kufuata taratibu kwa kutengeneza barabara za kisasa.Niwasihi TARURA m uwe wasimamizi wazuri wa ujenzi barabara kama wanavyofanya TANROAD ili tuwe na barabara zinazodumu muda mrefu," amesema Makonda.

MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika leo jijini.

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema(kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori wakiwa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es Salaam 


Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(kushoto) pamoja na wajumbe wakingine wakiwa kwenye kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...