NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’, ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Kada wake marehemu Mzee Abdulrazaq Mussa Simai 'Kwacha' aliyefariki  leo Machi 11,20118.

Mzee  Abdulrazaq  amefariki katika  Hospitali ya Kuu ya Taifa ya Muhimbili, iliyopo  Jijini Dar es salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika Salamu hizo Dk. Mabodi amesema CCM imepokea taarifa ya kifo hicho kwa mshutuko mkubwa na uzuni ya hali ya juu, kutokana na  marehemu Abdulrazaq alikuwa mwadilifu kwa Chama chake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wote wa uhai wake, na amemtaja kuwa ni miongoni mwa Wana ASP aliyeyalinda na kuyathamini Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa vitendo.

Kupitia salamu hizo Dk. Mabodi amewaomba  familia ya marehemu, Wanachama, Viongozi na Watendaji wote wa CCM, Marafiki, Ndugu  na Jamaa wote walioguswa na msiba huu kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu  na kuendelea  kumuombea dua.

Enzi za uhai wake Abdulrazaq amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ikiwemo Katibu Maalumu wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume.

Marehemu amezikwa leo katika kijiji cha Paje wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, amefariki akiwa na umri wa miaka 98 ameacha watoto watano  na  kizuka mmoja.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu pahala Pema Peponi Amin.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili leo katika maziko ya MarehemuMzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) Mwanasiasa Mkongwe wa CCM   katika Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) alijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali leo katika kumswalia  Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) Mwanasiasa Mkongwe wa CCM   katika  Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka udongo kaburini wakati wa maziko ya  Mwanasiasa Mkongwe wa CCM Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) baada ya kumswalia katika  Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
 Maelfu ya Wananchi kutoka sehemu mbali mbali za Zanzibar na Tanzania Bara walijumuika katika maziko ya Mwanasiasa Mkongwe wa CCM Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha)  yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Paje   Wilaya ya Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ( kulia) alifika kuwapa mkono wa pole Wanafamilia ya   Marehemu  Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) Mwanasiasa Mkongwe wa CCM  Nyumbani kwao baada ya mazishi yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja. Picha na Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...