WANACHAMA  3,500 wa Chadema katika Kijiji cha Narakauwo, Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro, wamejiunga na CCM kwa lengo la kumuunga mkono Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Manyara,  Alexander Mnyeti. 

Wananchi hao ambao awali walikuwa CCM, waliondoka kwenye chama hicho na kujiunga na Chadema, baada ya kigogo mmoja kukata majina ya baadhi ya wagombea waliokuwa wanawaunga mkono kwenye Kijiji hicho na kata hiyo mwaka 2015. 

Akizungumza jana wakati akiwapokea wanachama hao wapya kwenye mkutano uliofanyika kijiji cha Narakauwo, Mnyeti ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM Mkoani Manyara, alitoa onyo kwa wanasiasa wanaowayumbisha wananchi wa eneo hilo. 

Mnyeti alisema kuna baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo bado wamelala kwani wanadhani huu ni wakati wa kufanya siasa ili hali ilishakwisha mwaka 2015 na huu ni wakati wa kufanya kazi. "Kuna baadhi ya viongozi walikaa vikao usiku ili kukwamisha suala hili, nawapa onyo la mwisho, kama kuna mtu anataka ubunge asubiri mwaka 2020 siyo leo," alisema Mnyeti. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza na wananchi wa kijiji cha Narakauwo Wilayani Simanjiro juu ya mgogoro wa uongozi na kumuagiza mkuu wa Wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula aitishe kikao cha wanakijiji hao ili kujadili tatizo lao.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkoa huo, akimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Narakauwo, Saruni Ole Sanjiro kadi ya CCM kati ya wananchi 3,500 wa Chadema waliojiunga na CCM jana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...