Na Richard Mwaikenda
Tangazo la uuzaji wa mananasi limetolewa na Mkurugenzi Mtandaji wa Mkikita, Adam
Ngamange, ambaye hivi karibuni ameingia mkataba wa kuuza matunda hayo ndani na nje ya nchi.
Ngamange amewakaribisha Ofisi za Mkikita Dar es Salaam, wadau wenye maeneo ya kuuzia ili wapate utaratibu wa kununua jumla na kuyauza rejareja.
Bei ya mananasi hayo yaliyolimwa ki-organic kila moja huuzwa kwa bei ya kutupa ya sh. 1,200 itakayomwezesha muuza rejareja kupata faida kubwa.
Huduma hii inatarajiwa kuanza Machi 20 jijini Dar es Salaam, ambapo Mkikita imeingia mkataba wa kila wiki kuingiza sokoni nanasi 20,000.
"Hii ni fursa ya kuongeza kipato kwa wanaopenda kuwa wasambazaji na wenye mahoteli. Huu ndiyo mwanzo wa viwanda mkoani Njombe. Ungana na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania kuhamasisha kilimo mkataba," amesema Ngamange.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...