NA ELISA SHUNDA,MAFIA .
VIONGOZI wanaounda Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mafia wametakiwa kujitoa kwa nguvu,mali na rasilimali zao katika kukitumikia chama hicho na kuhakikisha kinafanya vizuri katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu 2020 ili CCM katika wilaya hiyo kiibuke na ushindi wa kishindo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Charangwa Selemani Makwiro wakati alipofanya ziara wilayani humo leo ambapo katika kuhakikisha vijana wa wilaya hiyo wananufaika na serikali ya Dk.John Pombe Magufuli amepata fursa ya kutembelea ofisi ya wilaya na halmashauri ambapo amekutana na uongozi na kupewa maelezo ya mnufaiko wa vijana wa Mafia katika asilimia 4% ya mikopo na miradi inayotolewa na uongozi huo kwa vijana hao.
Mwenyekiti Makwiro amewaeleza vijana hao kuwa wao ndiyo nguvu ya chama na kuwataka kusimama ngangari kama viongozi na vijana wa CCM kwa kutumia nguvu,mali,akili na rasilimali zao zote katika kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa mwakani wa serikali za mitaa ambapo ndiyo msingi wa ushindi wa uchaguzi mkuu wa madiwani,ubunge na urais hivyo ni jukumu lao vijana kukipigania chama katika maandalizi ya uchaguzi huo.
“nimefarijika siku ya leo kukutana na viongozi na vijana wa CCM wa Wilaya hii ya Mafia napenda kuwausia na kuwakumbusha vijana wenzangu mmeomba nafasi za uongozi kwenye maeneo yenu hivyo basi unapoomba nafasi katika chama hiki usitarajie labda kuna hela utapata au uwe kibaraka wa kiongozi Fulani ili maisha yako yaendelee hapana umeomba nafasi ya uongozi kwa ajili ya kuwatumikia vijana wenzako ni jukumu lako kama kiongozi sasa kutumia nguvu zako,akili,mali na rasilimali katika kukitumikia chama hiki;
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na viongozi na wajumbe chama hicho wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani leo,Kiongozi huyo yupo katika ziara ya kutembelea jumuiya za umoja wa vijana wa Mkoa huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mafia,Amina Tuki wengine kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango. Picha zote na Elisa Shunda
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...