Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Mkoani Rukwa wamesaini mikataba na wakandarasi 18 wa hapa nchini ili kufanyia matengenezo ya barabara za urefu wa kilometa 241.7 mkoani humo zitakazogharimu shilingi Bilioni 2.8.

Kati ya urefu huo barabara za kiwango cha lami kitakuwa ni km 1, changarawe km 77.91, udongo km 163.8 na kuweka alama za barabarani 123, ambapo pia kuna jumla ya vivuko 66 vitakavyotengenezwa vikiwa ni “drifts” 1 na makalavati ya aina mbalimbali 65.

Katika kutekeleza hilo TARURA ilizingazia kutoa kipaumbele kwa wakandarasi waliomo Mkoani Rukwa, na kati ya wakandarasi 18, 12 ni wakandarasi wa mkoa wa Rukwa ambao wanafanya asilimia 67 ya wakandarasi wote.

Awali akitoa hutuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa Benard Makali ameasa kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa kazi zinazofanyika ili zifanyike kwa kiwango kinachokubalika na kuhakikisha malipo yanafanyika kwa wakati ili kuwawezesha wakandarasi kukamilisha kazi kwa wakati.

“Serikali iko macho na haitasita kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi yeyote atakayebainika kuwa ameenda kinyume na matarajio ya serikali hii ya awamu ya Tano na kuuchafua Wakala huu na Serikali kwa ujumla kwa vitendo visivyo vya kimaadili.” Makali alisisitiza.
 Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali akikabidhi mmoja wa mkataba kwa mmoja wa Wakandarasi hao Luis Mamba muda mfupi baada ya kusaini mikataba hiyo. 
  Mwanasheria wa TARURA Mkoa wa Rukwa, Jery Simon akisaini miongoni mwa mikataba 18 iliyosainiwa na kukabidhiwa kwa wakandarasi. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...