Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeendelea na zoezi la Usajili
Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Tabora, ambapo Wilaya
zote zinaendelea na zoezi hilo.
Akizungumzia mwenendo wa zoezi hilo Afisa Usajili Mkoa wa Tabora Bi Grace Msaky, amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa na kwamba wananchi wameelewa umuhimu wa Vitambulisho.
Amesema; kuhakikisha wananchi wanapata huduma na wanafikiwa mahali walipo kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa sasa zoezi wanaendesha kwenye Vijiji na Mitaa wanakokaa wananchi na kwamba wananchi wanajulishwa muda na wakati wa kufika kwenye vituo kupata huduma hiyo.
“ kwa sasa wananchi wanaelewa utaratibu; ila changamoto ni baadhi ya wananchi kufika siku za mwisho wa zoezi na kufanya zoezi kuchukua muda mrefu kwenye baadhi ya Kata kinyume na ratiba iliyopangwa” alisisitiza.Mbali na Tobora mikoa mingine 19 inaendelea na zoezi kwa Tanzania Bara huku Tanzania Zanzibar zoezi hilo likiwa limekamilika kwa asilimia 99%.

Wananchi wa kata ya Ipuli mtaa wa Ipuli Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye mashine maalumu za uchukuaji taarifa muhimu za Usajili zikiwemo upigaji picha, alama za vidole na saini ya kielektroniki.
Mkazi wa Mtaa wa Ipuli Bi Halima Abed akiwa kwenye zoezi la kupigwa pichwa ili kukamilisha Usajili

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...