Benki ya CRDB leo imetangaza kuanza
rasmi kwa kampeni ijulikanayo kama “Furahia kandanda murua nchini Urusi”
#TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiaji wa kadi za malipo za TemboCard
Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe
la Dunia zitakazofanyika nchini Urusi, kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi
wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo Bi. Tully Esther Mwambapa,
alisema kuwa Benki ya CRDB imeanzisha kampeni kwa kushirikiana na kampuni ya
Visa International ili kutoa fursa kwa wateja wake kwenda kushuhudia fainali hizo,
ambazo huvutia hisia za watu wengi dunuani kote.
“Wateja wetu wenye
TemboCardVisa, TemboCardVisa-Electron, TemboCard Visa-Gold, TemboCardVisa-
Platinum na TemboCardVisa-Infinite, wakati wa kampeni hii watatakiwa kulipia bidhaa
au huduma wanazonunua kwa kutumia TemboCardVisa zao kupitia mashine za malipo
(POS) zilizopo sehemu mbalimbali kama kwenye migahawa, maduka, mahospitali, vituo
vya mafuta na kwingineko, ili waweze kujishindia zawadi hii kubwa” alisema.
Bi.Mwambapa aliendelea kusema kuwa “iii mteja aweze kushinda, anatakiwa kufanya
miamala mingi zaidi kila wiki na kadri mteja anavyolipia zaidi kwa kutumia
TemboCardVisa yake, ndivyo anavyojiongezea nafasi kubwa zaidi ya kushinda.
Washindi wa wawili watakaokuwa wamefanya miamala mingi zaidi kila wiki
watajishindia safari ya kwenda Urusi ambayo itagharamiwa kila kitu na Benki ya CRDB,
ambapo jumla ya tiketi 24 zitatolewa” alisema Bi. Tully Mwambapa.
Bi.Mwambapa aliendelea kusema kuwa pamoja na washindi wawili wa kwanza
kujishindia safari hiyo, Benki pia kila wiki itatangaza washindi wengine 10 kupitia
vyombo mbalimbali vya habari ambao watajishindia zawadi kemkem ikiwemo luninga
zitakazokuwa zimeunganishwa na kulipiwa kinga’muzi cha DSTV, jezi za timu za
mataifa mbalimbali, mipira, kofia, fulana na na zawadi zingine nyingi.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akionyesha vipeperushi vya kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitangaza kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...