KATIKA hali isiyo ya kawaida mkazi wa Kijiji cha Bulambizi katika Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera Respicius  Diocless anadaiwa kuwaua watoto wake wawili ambao ni mapacha kwa kuwachinja kwa kuwatenganisha vichwa na viwiliwili.

Watoto hao wamefahamika kwa majina Deonidas Respicius na Diocress Respicius (wenye umri wa miaka 4) ambapo tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumapili ya  Aprili 15 mwaka huu.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambae pia ni mtoto mdogo wa kumzaa, Kelvin Respicus amedai baba yake mzazi aliwachukua watoto hao kwa zamu na kisha kutelekeza mauaji hayo."Nilipojaribu kuhoji wapi ndugu zangu alinijibu wapo mbinguni,"amedai.

Taarifa zaidi zinadai kbla ya tukio, mtuhumiwa alikuwa akiishi na watoto wake watatu wakiwemo mapacha hao ambao amezaaa na mwanamke anayejulikana Deovitha David ambaye kwa sasa wamekwishaachana.

Inadaiwa kabla ya kufikwa na umauti mama wa watoto hao aliwaomba awachukue kutoka kwa mzazi mwenzie 

na ombi hilo lilikubaliwa kwa sharti ya kuwarudisha kwake Jumamosi.

Hivyo aliwachukua na kuwarudisha siku hiyo na kisha mwanamke huyo aliondoka.Hata hivyo usiku ndipo sasa mtuhumiwa huyo (baba mzazi wa watoto)anatuhumiwa kufanya tukio hilo la kinyama.

Kutokana na mauaji hayo, hadi sasa hakuna anayejua sababu iliyomfanya mtuhumiwa kuua wanawake mapacha, ingawa wapo wanaodai kuna mgogoro unaosababisha na mapenzi uliokuwa ukiendelea kati ya wanandoa hao.

Juhudi za kupata ukweli wa sababu za mauaji hayo hadi sasa hazifanikiwa kwani hata mama watoto hao wameshindwa kuzungumza chochote kutokana na huzuni aliyonayo ya kupoteza watoto wake.

HOFU YA WANAKIJIJI

Inaelezwa baada ya kutokea tukio hilo usiku, ilipofika asubuhi mtoto alikuwa wa kwanza kutoa taarifa za mauaji hayo kwa ndugu, jamaa na marafiki.Hivyo taarifa zikafikishwa kwa Mwenyekiti wa kijiji Bulambuzi.

Baada ya taarifa kusambaa kuhusu mauaji hayo mtuhumiwa alifanikiwa kukimbia kusikojulikana na taarifa nyingine zikadai bado yupo kijijini hapo.

Hata hivyo wananchi waliamua kuchoma nyumba yake na kisha kuendelea na msako ili kumtia mikononi na sheria ichukue mkondo wake.

Wakati wana kijiji wakiendelea kumsaka, mtuhumiwa anadaiwa kutumia simu yake ya mkononi kutuma ujumbe mfupi kupitia simu yake na hata kupiga simu akitaka wqasihangaike kumtafuta kwani amefanya tukio hilo akiwa na akili timamu.

Pia kupitia simu yake anawaambia wanakijiji ambao anawatumia ujumbe na kuwapigia kuwa akikamilisha azma yake basi atajisalimisha kwenye vyombo vya dola.

Pamoja na kutuma ujumbe kupitia simu yake, tayari mtuhumiwa huyo amekamatwa jijini Mwanza na kinachoendelea ni kumfikisha mahakamani sheria ichukue mkondo wake.

Kwa hisani ya Bukobawadau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...