Majeneza yenye miili ya Mapadri watatu wa kanisa katoliki jimbo la Same ambao vifo vyao vilipishana kwa siku moja moja, yakiwa katika Seminari ya Chanjare wilayani Mwanga kwa ibada ya Mazishi. Mapadri waliofariki dunia ni Padri Michael Kiraghinja (11/04/2018), Padri Arbogast Mndeme (12/04/2018) na Padri Ulbadus Kidavuri (13/04/2018). Ibada ya mazishi inaongozwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa katoliki, Askofu Josephat Lebulu.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira (wa pili kulia) , Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Senyamule pamoja na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah wakiwa wameungana na waumini pamoja na waombolezaji wengine katika Misa hiyo ya Mapadre watau wa kanisa katoliki jimbo la Same ambao vifo vyao vilipishana kwa siku moja moja, inayoendelea kufanyika hivi sasa katika Seminari ya Chanjare wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...