Mpango wa Pizza Hut wa Elimu wa Afrika Kuletwa Tanzania
Chapa kubwa ya Pizza duniani yabadili boksi zake kuwa boksi nyenkundu za kujisomea kama mradi wake wa kuhamasisha watoto kusoma duniani
KAMPENI mpya inayosafiri ya Pizza Hut Afrika inayohamasisha kusoma kwa watoto imefika jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inayoenda kwa jina la ‘Kipande cha Afrika (Slice of Africa)’ inaongozwa na Meneja Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport na timu yake ambayo wanasafiri katika miji 14 na nchi 12 barani Afrika kufuatia mchoro wenye umbo la kipande kikubwa cha chakula aina ya pizza.
“Badala ya kusambaza pizza tunasambaza viboksi vya rangi nyekundu (Red Reading Boxes) tukishirikiana na shirika lisilo la kiserikali ‘READ Educational Trust’, katika kutafuta njia za kivumbuzi za kuendeleza elimu kwa ajili ya watoto katika kila nchi,” alisema Davenport.
“Kutokana tafiti zinazosema kwamba zaidi ya watoto milioni 280 barani Afrika hawajui kusoma, kampeni hii ni muhimu sana. Elimu na kujisomea ni fursa kubwa katika kuleta maendeleo na tumelenga kutumia ukuaji wa migahawa yetu barani Afrika ili kuleta mabadiliko katika jamii tunazotumikia.”
Katika safari yao timu hiyo ya ‘Slice of Africa’ ikiwa na wafanya biashara wa kampuni hiyo ya Pizza Hut watazindua kampeni ya kujitolea kwa wateja katika kila nchi ili kukusanya fedha zitakazojumuishwa na za kampuni hiyo ili kuweza kusambaza maboksi mengi zaidi.
Meneja Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport (kushoto) akiwa na watoto kutoka Shule ya Msingi ya Nzinga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuhamasisha watoto kusoma na kuandika wa Kiafrika ambapo walipewa boksi nyenkundu zenye vifaa mbalimbali vya kusoma na kuandika. Kampeni hii ni mradi wa kijamii wa kampuni hiyo ulioanzishwa mwaka 2016. Mradi huu uliundwa ili kuhamasisha elimu kupitia utoaji wa rasilimali na kushirikisha wateja ili kuleta mabadiliko katika jamii.
Meneja Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport (kushoto) akionyesha vifaa ambavyo vitakuwa kwenye mradi wao mpya uitwao "Red Reading Boxes" kwa ajili ya kuhamasisha watoto kusoma na kuadika. Kampeni hii ni mradi wa kijamii wa kampuni hiyo ulioanzishwa mwaka 2016. Mradi huu uliundwa ili kuhamasisha elimu kupitia utoaji wa rasilimali na kushirikisha wateja ili kuleta mabadiliko katika jamii.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...