Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Msanii
mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto anatarajia
kupelekwa nchini India kwa matibabu kutokana na tatizo linalomkabili.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya
kutoka kumsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya
Tumaini, Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere'
amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona mzee Majuto amekuwa
akihangaika mara kwa mara kutafuta matibabu.
"Tumeona
mzee wetu anahangaika na matibabu ya mara kwa mara ambayo hayakamiliki
sasa tumekuja na wazo la kumpeleka nchini India ili akatibiwe tatizo
lake liishe na huu ndiyo wakati mwafaka wa watu tujitoe si mpaka mtu
ashindwe kuongea tuanze michango," alisema nyerere.
"Jamani ifike wakati tujitoe kumsaidia mtu akiwa yupo hai na tusisubiri
afariki ndiyo tuanze kuchanga, wakati ni sasa akiwa anaumwa tunamchangia
anapatiwa matibabu na anaendelea na maisha," amesema Nyerere.
Tunamshukuru
Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuunga mkono
kusaidia mwenzetu, pia Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taiga (NEC)
Salim Asas ambaye yeye amesema atatusaidia kwa hali na mali na ameanza
kutupa tiketi 2 za ndege.
Tunataka mwenzetu akatibiwe maradhi yake yaishe aendelee na majukumu
yake ya kujenga nchi na familia yake kwa ujumla.
Nyerere
amewaomba wadau mbali mbali akiwemo Azam, DSTV na wengine wote wenye
mapenzi mema kumsaidia mzee Majuto ili apone na aendelee na shughuli.
Kwa Upande wa Mzee Majuto amewashukuru watu wote ambao wamekuwa
wakijitokeza kumsalimia na waendelee kumuombea ili apone.
"Sina cha kuwapa zaidi ni kuwaombea muendelee na moyo mlionao, mimi sina
pingamizi kwenda kutibiwa nchini India, nipo tayari kamilisheni mipango
yote mje kunichukua," amesema.
Ujumbe wa Steve Nyerere uliambatana na msanii mwenzake Aunty Ezekiel pia
wakiwemo na waandishi wa habari wa mitandao ya jamii.
Msanii Aunty Ezekiel akimsalimia Mzee Majuto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...