Na Anitha Jonas – WHUSM
Utendaji uliyotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious Awards.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana katika tuzo hizo.
“Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, napia tuna wasanii watatu ndani ya tansia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika,Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika,”alisema Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika sherehe hiyo ya kukabidhi bendera Mheshimiwa Mwakyembe aliwasisitiza wasanii wanchini kuendelea kuandaa kazi zinazoonyesha ubunifu wao kwani ukuaji wa tansia ya filamu Tanzania uko mikononi mwao na si vinginevyo.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (watatu
kushoto) akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie
maarufu kama Monalisa jana jijini Dar es Salaam anayetarajia kwenda
nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious
Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike
Afrika,wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa
Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (wapili
kushoto) akimkabidhi Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu
kama Monalisa tiketi ya ndege jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
safari yake ya kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The
African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha
Msanii Bora wa Kike Afrika,kutoka kulia wapili ni Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kulia ni
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania Bw.Godfrey Mngereza.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(wakwanza kushoto)
akifafanua kwa waandishi wa habari na wadau wa sanaa (hawapo pichani)
kuhusu tuzo za The Africa Prestigious Awards jana jijini Dar es Salaam
zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni kwa kueleza heshima ya tuzo
hizo na Tanzania imepata heshima ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli nae kuteuliwa kuwania tuzo
ya kiongozi bora Afrika,wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.
Msanii
wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa akiahidi kwa
Waziri wa habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe
(hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam katika sherehe ya
kukabidhiwa bendera kuwa atarudi na tuzo hata kama yeye hatopata basi
ataweza na kurudi na hata tuzo ya Msanii Raymond Kigosi anayewania Tuzo
ya Msanii Bora wa Kiume Afrika au Tuzo ya Msanii King Majuto anayewania
Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika au Mpiga picha Moiz Hussein anayewania
Tuzo ya Mpiga picha Bora Afrika katika tuzo za The African Prestigious
Awards zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni,wa kwanza kulia ni
Mama Mzazi wa Msanii Monalisa Bibi Suzan Lewis maarufu kama Natasha.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...