Kiongozi
wa mbio za mwenge,Charles Kabeho akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa
mradi wa maji wa Kasanda iliofadhiliwa na Water Mission Tanzania.
Shamrashamra za uzinduzi wa mradi
Kiongozi
wa mbio za mwenge, Charles Kabeho, akiongea na wananchi wakati wa
uzinduzi wa mradi wa maji Kasanda,(kushoto) ni Mkurugenzi wa Kanda wa
shirika la kimataifa la Water Mission, Will Furlong
Shirika la kimataifa la Water Mission Tanzania lafanikisha mradi wa maji
safi na salama katika Kijiji cha Kasanda
Wakazi wa kata ya Kasanda, wilayani Kakonko mkoani Kigoma, jana,wameanza
kupata maji safi na salama kutokana na kuzinduliwa kwa mradi mpya wa
maji chini ya ufadhili wa Shirika la kimataifa la Water Mission
Tanzania.
Mradi
huu utanufaisha zaidi ya kaya 729 zinazoishi maeneo hayo.
Miradi ya Kakonko na Kasanda, ni miongoni mwa miradi zaidi ya 20 ya
kuwapatia wananchi maji safi na salama ambayo imetekelezwa na shirika la
Water Mission Tanzania tangu mwaka 2014. Miradi ya Kasanda na Kakonko
ni tofauti na ile iliyotekelezwa maeneo mengine kwa kuwa iko katika
maeneo yaliyopo karibu na kambi ya wakimbizi ya Mtendeli.
Mkurugenzi
wa Kanda wa shirika la kimataifa la Water Mission, Will Furlong alisema
“Water Mission Tanzania, kupitia ufadhili wa taasisi ya Poul Due Jensen
Foundation ambayo zaidi inajulikana kama, Grundfos Foundation,
imewezesha ufanikishaji miradi 8 ya maji safi na salama kwa jamii
mbalimbali nchini.
Mradi
mwingine wa Zeze mkoani Kigoma nao tayari umezinduliwa mwezi huu.
Mashirika ya Water Mission Tanzania na Grundfos Foundation,
yanashirikiana kuhakikisha huduma za maji safi na salama zinafikia jamii
zenye changamoto katika kanda ya Afrika Mashariki”.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa mradi huu mkubwa wa maji ulioambatana na sherehe
za mbio za Mwenge katika kata hiyo,Kiongozi wa mbio za mwenge,Charles
Kabeho,alisema kuwa kuzinduliwa kwa mradi huo ni jambo la kihistoria kwa
wakazi wa eneo hilo ambalo kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto ya kupata maji safi na salama.
“Kwa
niaba ya serikali napenda kutoa shukrani kwa wadau wa maendeleo
wanaounga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto
mbalimbali zinazokabili jamii kama ambavyo hawa wenzetu wa Water Mission
Tanzania ,wamekuwa mstari wa mbele kufanikisha miradi ya maji sehemu
mbalimbali hapa nchini”alisema Kabeho.
Alisema
kero ya ukosefu wa maji safi na salama kwa muda mrefu ilisababisha
akina mama kutembea mwendo mrefu kutafuta maji sambamba na wananchi
wengi kuathirika kwa kupata magonjwa mbalimbali kutokana na kutumia maji
yasio salama kwa matumizi ya binadamu.
Kabeho,alitoa wito kwa wakazi wote wa eneo hilo kujiona ni sehemu ya
mradi huu na kuhakikisha wanatunza miundo mbinu ya mradi wakati wote
sambamba na kutoa ushirikiano kwa wataalamu wanaofanya ushauri wa
uendeshaji mradi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...