Na Stella Kalinga, Simiyu.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) Awamu ya tatu umeendelea kunufaisha wananchi wakiwemo wakazi wa
kijiji cha Nkoma wilaya ya Itilima na Nyakabindi wilaya
ya Bariadi mkoaniSimiyu.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango
huo, Bibi. Rebecca Masunga kutoka Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi,
amesema TASAF imemsaidia kutoka katika umaskini sasa anapata kipato
kinachomwezesha kujikimu, kwa kuwa amelima ekari tatu za pamba, ekari
moja ya mahindi, ana ng’ombe 14 na mbuzi wanne na amenunua plau kwa
ajili ya kulimia.
“Nilikuwa maskini wa kutupwa ,
nilipoingia TASAF na kuanza kupokea zile elfu 36 nilikopa fedha nikalima
nyanya ekari moja nikauza, nilipata shilingi laki sita nikanunua
ng’ombe watatu wakakua; baadaye nikawauza nikapata milioni moja na laki
tano nilinunua ng’ombe 14 ndiyo hao mnaowaona tunawachunga sasa”
alisema Rebecca Masunga
“Tuna kikundi chetu ambacho
tunaweka fedha zetu baadaye tunagawana, tukisha gawana tunaenda
kuzalisha, tunalima nyanya, kabeji, pamba halafu tunauza; mpango wangu
wa baadaye niwe na mtaji mkubwa na nijenge nyumba bora ” alisisitiza
Bibi.Masunga.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakikagua shamba la pamba la mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga (mwenye kitambaa cheupe kichwani) wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia mifugo ya mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akimpongeza mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi kwa kununua jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau) kwa ajili ya kulimia, wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu walipotembelea na kuona nyumba ya mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Stella Masamaki wa Mtaa wa Old Maswa wilayani Bariadi, wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...