Kiongozi wa Msafara wa wachezaji waliyokwenda katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Australia ambaye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo akizungumza na kwa waandishi wa habari (hawapo picha)kuhusu hali ya mashindano pamoja na suala la mchezaji mmoja kutoroka kambini mara baada ya kuwasili nchini leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa Jijini Dar es Salaam.
Bondia Selemani Kidunda (wa kwanza) akiwasilini leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea nchini Australia ambapo alikwenda kwa ajili ya Mashindano ya Jumuiya ya Madola nyuma yake ni Bondia mwenzie Haruna Swanga.
Mwanariadha wakike Bi.Sara Ramadhani akiwa amewasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo akitokea nchini Australia ambapo alikwenda katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola na ameshika nafasi ya tisa katika mbio za Kilometa 42.
Kapteni wa Timu ya wachezaji waliyokwenda nchini Australia katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola Bw.Masoud Mtalaso (kulia) akirejesha bendera aliyokabidhiwa wakati wanakwenda katika mashindano kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Alex Nkenyenge (kushoto) mara baada ya kurejea nchini leo jijini Dar es Salaam. Na Anitha Jonas – WHUSM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...