Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA) imesema katika kipindi cha
miezi 9 ya mwaka wa fedha 2017/2018 kuanzia Julai 2017 hadi
Machi mwaka huu wamekusanya Sh.Trilioni 11.78.
Akizungumza Dar es Salaam leo ,Mkurugenzi wa Huduma na Elimu
kwa Mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema makusanyo hayo
yameongezeka ikilinganishwa na Sh.Trilioni 10.86 zilizokusanywa
kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha was 2016/17.Kiasi hicho in
sawa na ukuaji wa asilimia 8.46.
"Katika Machi mwaka 2018 pekee TRA imekusanya jumla ya
Sh.Trilioni 1.54 ikilinganishwa na makusanyo ya Machi mwaka 2017
ambapo ilikusanywa Sh.Trilioni 1.34 ambayo ni sawa na ukuaji wa
asilimia 14.49," amesema Kayombo.
Amefafanua kufanikiwa Katika makusanyo hayo yametokana na
walipa kodi ,viongozi wa ngazi zote na wananchi pamoja na kampeni
kadhaa tunazofanya ikiwamo ya usajili wa walipa kodi nchi nzima.
Pia TRA inaendelea kuwakumbusha walipa kodi kulipa kodi kwa
wakati ,kusikiliza malalamiko pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa
kulipa madeni ya nyuma.
Amefafanua kipindi hiki wanaendelea na usajili wa walipakodi
wapya wakiwemo wamachinga ambapo kwa wiki hii wapo mkoa
wa Geita.
"Tunawakarabisha wafanyabiashara wa mkoa wa Geita kujitokeza
kusajiliwa na kupata namba ya utambulisho ya mlipakodi (TIN) na
pia kutoa kero zao kwa maofisa wa mamlaka ili wasikilizwe na
kuhudumiwa.
"Pia nachukua fursa hii kuwakumbusha wananchi Aprili hadi Juni ni
robo ya mwisho ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa hiyo walipe
kodi ya majengo ambayo kwa sasa unaweza kulipa kwa njia ya
mtandao kwa kutumia simu ya mkononi kwa kupiga *152*00# na
kufuata maelekezo,"amesema Kayombo.
Amesema wanaendelea kutoa elimu ili kila anayestahili alipe kodi
kwa hiari na kwa wakati na mwenye malalamiko yoyote ya
makadirio amuone meneja wa eneo husika na vilelezo vyote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...