Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Shinyanga

CHUO cha Ufundi Stadi (VETA)Mkoa wa Shinyanga kimeanzisha na kuendeleza mafunzo ya kozi yenye kulenga kuzalisha nguvukazi yenye ujuzi wa kusaidia sekta za madini, ujenzi, kilimo na misitu. 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Afridon Mkhomoi wakati anazungumza na waandishi habari waliotembelea katika chuo hicho leo.Amezitaja kozi zilizoanzishwa katika mwelekeo wa kusaidia sekta hizo ni ukataji na ung’arishaji madini ya vito, ufundi wa mitambo mikubwa,uendeshaji wa mitambo mikubwa na upasuaji miamba.

Amesema chuo cha VETA Shinyanga kina kozi ambazo zina uwigo mkubwa wa ajira katika uchimbaji wa madini, ujenzi, kilimo na misitu, lakini bado idadi ya vijana wanaojiunga ni ndogo.

Aidha amesema mwitikio wa wananchi wenyeji wa Mkoa wa Shinyanga kusoma katika chuo ni mdogo zaidi, hivyo kufanya chuo hicho kudahili zaidi wanafunzi kutoka mikoa mingine.Hata hivyo, kozi ya uendeshaji wa mitambo mikubwa imeonekana kuvutia vijana wengi wakiwemo wasichana na kwa mwaka huu, kozi hiyo ina jumla ya wanafunzi 149.

Ambapo wapo wa mafunzo ya muda mrefu wa miaka miwili na muda mfupi wa miezi miwili. Kati ya wanafunzi hao, 11 ni wasichana.Mmoja wanafunzi wa kozi hiyo, Happiness Mposola amesema amevutiwa na kozi hiyo na kuamua kujiunga nayo licha ya mtazamo uliokuwepo kwa muda mrefu kuwa hiyo ni kozi kwa ajili ya wanaume.

Amesema sasa ni wakati wa wanawake kuamka katika kuchangamkia fursa mbalimbali kwani hakuna kazi alizopangiwa mwanaume au mwanamke pekee, bali kazi zote zinaweza kufanywa na wanaume na wanawake.

Kwa upande wa Mratibu wa Mafunzo wa Chuo hicho, Magu Mabelele amesema, kozi hiyo imevutia hata vijana kutoka nchi zingine za Afrika."Katika kipindi cha miaka miwili tumekupokea wanafunzi kutoka nchi za Rwanda, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi," amefafanua.
 Mkuu wa Chuo cha VETA  Shinyanga, Afridon Mkhomoi akizungumza na waandishi habari walipotembelea chuo hicho kuhusiana na fursa ambazo zinapatikana katika chuo.

02.Mwanafunzi wa Uendeshaji wa Mitambo, Happiness Mposola akizungumza kuhusiana na kozi uendeshaji matambo alivyojipanga.

03.Mwanafunzi wa Veta Shinyanga katika kozi ya Uendeshaji na  Mitambo, Happiness Mposola akiendesha Escaveter ikiwa sehemu ya kozi hiyo.

04.Mwanafunzi wa kozi ya Ukataji na Ungalishaji wa Madini ya Vital, Jeta Giga akingalisha madini ya vital katika mitambo.
.Wanafunzi wa Chuo cha VETA wa wakionesha ujuzi katika kufungua Injini nza mitambo.

Mkufunzi wa Kozi ya Salon na Mapambo, Juddy Marcus akizungumza kuhusiana na kozi ya salon na mwitikio kwa vijana kujifunza kozi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mm nina miaka 39 sina elimu yeyote nanina ada naruhusiwa kujifunza

    ReplyDelete
  2. Mm nina miaka 39 na sina elimu yeyote ninayo ada iliyokamilika naruhusiwa kujifunza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...