Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), wameshiriki kuchangia damu kwa lengo la kusaidia wenye uhitaji wa damu nchini ili kunusuru maisha yao.

Tukio hilo la wafanyakazi hao kuchangia damu limefanyika leo kwenye moja ya viwanja vyao vilivyopo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza wakati wa uchangiaji damu katika Maadhimisho ya 13 tangu  kuanzishwa TPA, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari (Dowuta), Mashaka Karume amesema maadhimisho hayo ni daraja la kuwakutanisha wao na jamii kwa kutoa msaada sehemu mbalimbali likiwemo hilo la kuchangia damu.

Karume amesema maadhimisho ya hayo ni sehemu ya kukutana na menejimenti nje ya kufanya kazi  lakini tunashirikiana katika masuala ya kijamii.

"Maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa mamlaka ya bandari kama wafanyakazi tunaona mafanikio ambayo ni pamoja na mamlaka kushiriki kutoa msaada pamoja na hili la uchangiaji damu,"amesema Karume
 Wafanyakazi wa TPA wakijiandaa katika uchangiaji damu katika viwanja vya bandari ikiwa ni maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafayakazi wa Bandari, Mashaka Karume akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uchangiaji damu katika maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafayakazi wa Bandari, Mashaka Karume akiwa katika picha pamoja na wafanyakazi wa mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...