Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee ambaye pia ni Mwenyekiti wa The Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya Ziwa akisisitiza jambo katika ibada iliyofanyika katika Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Bwiru jijini Mwana, mwenyekiti huyo na waumini baadhi ya dini ya Kiislamu waliakwa kushiriki kwenye ibada hiyo ambayo imeandika historia mpya baina ya Waislamu na Wakristo kuwa wote ni wamoja na wanamuabudu Mungu mmoja.Kutoka kushoto wa pili ni Kaimu Katibu Mkuu wa kanisa hilo Philipo Majuja.

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WAISLAMU wa madhehebu ya Shia Ithna Asheri Imamia wamesema kitendo cha Wakristo wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) cha kuwaalika kushiriki Ibada kanisani kimefungua ukurasa mpya kwa waumini wa madhehebu hayo nchini.

Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) Tawi la Tanzania Alhaji Sibtain Meghjee ametoa kauli hiyo juzi katika Ibada iliyofanyika katika Kanisa la AICT Bwiru jijini Mwanza ambapo alikabidhi fimbo 11 kwa walemavu wa macho,vitabu vya Kuran na kalenda kwa waumini wa kanisa hilo.

"Mambo mengi yaliyopo kwenye Biblia na Kuran asilimia 90 yanafanana na kinachotakiwa kwa waumini wa dini zote za Kikristo na Kiislamu ni kuvumiliana kutokana na imani zao na hivyo ushirikiano huo utadumisha amani na utulivu kwenye jamii bila kubaguana kwa kutofautiana kiimani,"amesema.
Sheikh wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Sheikh Hashim Ramadhan akitoa neno kwa waumini wa kanisa la AICT Bwiru wakati wa ibada iliyowashirikisha pia waumini wa dini ya Kiislamu akisema wote ni watoto wa baba na mama mmoja na wanamwabudu Mungu mmoja na hakuna sababu ya kuchukiana bali kupendana.

Meghjee ambaye pia ni Mwenyekiti wa The Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya Ziwa amesema wapo baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa wakieneza propaganda chafu dhidi ya Uislamu wakiwahusisha na mambo mabaya kwenye jamii na kuipongeza serikali kwa kuanzisha kamati ya amani Mkoa wa Mwanza na kuufanya kuwa wa jamii moja bila kubaguana.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...