Na Joseph Mpangala-Mtwara
Shirika la Kuhifadhi mazingira duniani WWF imezindua Mradi wa Kuleta mabadiliko katika usimamizi na Uendelezaji wa Maliasiri za misitu,wanyapori na bahari kwa kushirikisha Asasi za Kiraia pamoja na Wananchi katika mikoa ya Kusini.
Mradi huo wa miaka mitano unagharimu zaidi ya shilingi Billion10 fedha ambazo ni msaada kutoka shirika la maendeleo la SIDA kutoka Nchini Sweden kwa lengo la kusaidia Serikali na wananchii katika Kuboresha Usimamizi wa maliasili.
Akiongea katika Uzinduzi wa Mradi huo Mkurugenzi wa shirika la WWF hapa Nchini Dk.Amani Ngusaru amesema katika Mradi Utawezesha akina mama na Vijana ili kuhakikisha wanachochea mabadiliko katika katika usimamizi wa maliasili kwa ajili ya matumizi ya Vizazi vya sasa na Vijavyo.
Dr.Amani ameongeza kuwa Bado Maliasiri zetu zinakabiliwa na Changamoto ya Uharibifu unaochangiwa na Ongezeko la Shughuli za kibinadamu.
“katika hivi karibuni kumekuwepo na uvamizi mkubwa wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya shughuli za Kilimo,Malisho ya Mifugo,Uchimbaji wa madini,ukataji wa miti mjanga ya moto pamoja na uvunaji wa misitu ya asili kwa ajili ya ujenzi”amesema Dk.Amani.
Mradi huu unaafanyakazi katika mikoa ya Lindi,Rumuma pamoja na mtwara.
Mkurugenzi
wa WWF hapa nchini Dr.Amani Ngusaru akiongea na wawakilishi wa asasi
mbalimbambali za kiraia wakati wa uzinduzi wa Mradi wa uendelezaji
Maliasili Mkoani Mtwara. 

.Kaim
Mkurugenzi wa Tunduru Jonathan A Haule wakatikati akionesha Kitabu cha
WWF mara baada ya kufanya Uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji wa maliasi
katika mikoa ya kuzini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...