Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
JAJI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Ibrahimu Juma, amefungua mafunzo elekezi kwa majaji wapya 14 wa Mahakama Kuu nchini yenye lengo la kuwataka kufanya kazi kwa makini kwa kuwa jamii inamatarajio makubwa kutoka kwao.
Mafunzo hayo ya wiki tatu yamezinduliwa leo katika kituo cha mahakama cha mafunzo ya uongozi kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mafunzo hayo yanahusu masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Tehama) hasa katika eneo la makosa ya kimtandao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hao Jaji Mkuu, amewataka majaji hao kutambua kuwa kadri wananchi wanavyotambua haki zao, mlundikano wa kesi unaweza kuongezeka lakini hiyo isiwe kigezo cha wao kushindwa kukidhi matarajio ya wananchi ya kusikiliza mashauri yao na kuyatolea maamuzi kwa wakati.
" Kwa sasa ninyi ni mali ya jamii na jamii inawaangalia na kuwa na matazamio ya kutatua kesi ambazo ziko mbele yenu kwa hiyo muwe mameneja wazuri ", amesema.Pia amewataka majaji hao kujiangalia na kuutumia muda wao vizuri na kuongeza "Kwanza tuna upungufu mkubwa wa majaji, na unapofanikiwa kupata majaji 12 unataka majaji wenye afya na wataofanya kazi sehemu yeyote katika Jamuhuri yetu sehemu yoyote watakayopangiwa, watafanya bila malalamiko kwamba
wanaugua.
"Sasa kuna magonjwa nyemelezi ambayo yanatokana na maisha, sasa tunawaambia wajiepushe na magonjwa hayo ili wawe na muda mwingi zaidi wa kufanya kazi za kimahakama badala ya kuwa na muda mwingi wa kwenda India au kuwa kwenye hospitali."
Akizungumza kuhusu mlundikano wa kesi, Jaji Mkuu amewataka majaji hao kujitahidi kuamua kesi ambazo zinaweweza kutolewa uamuzi mapema na kumalizika na kwamba jaji mmoja anaweza kuwa na kesi 500 lakini akashauri isiwe sababu ya kurundikana kwa kesi hizo.Ameongeza kuwa kwa sasa ukiiangalia jamii imebadilika na hivyo hawawezi kuacha hukumu zibaki kwenye makaratasi tu, bali hukumu hizo zitolewe mara moja na zipatikane kwenye mitandao.
Majaji wanaohudhuria mafunzo hayo ni, George Masaju, Gerson Mdemu, Ilvin Mgeta, Elinaza Luvanda, Joseph Mlyambina, Immaculate Banzi, Mustapher Siyani, Paul Ngwembe, Agnes Mgeyekwa, Stephen Magoiga, Thadeo Mwenempazi, Butamo Philip, Aziza Suwezi na Khamis Ramadhani..
Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa ili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Jaji Mstaafu, Mhe. John Mrosso, wa tatu kushoto ni Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, wa tatu kulia ni Mhe. Jaji Beatrice Mutungi, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wa pili kulia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo na Wahe. Majaji wa Mahakama Kuu.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, akitoa hotuba ya ufunguzi katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Zanzibar, Mafunzo hayo yamfunguliwa rasmi mapema Mei, 07, 2018 katika Ukumbi mpya wa Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu-Dar es Salaam.
Sehemu ya Wahe. Majaji wapya wakiwa katika hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo kwa Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania yaliyofunguliwa rasmi na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma
Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akitoa neno katika ufunguzi wa Mkutano huo.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto, Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo akiongea jambo katika hafla hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...